''UJIO MPYA WA DANNY BANDEZU UNALENGA KUTUMBUA MAJIPU KWA MUZIKI WA INJIRI''

DANNY BANDEZU': mwonekano wa mbele wa cd yake mpya inayoenda kwa jina la #sinyamazi
Danny Bandezu ni jina linalovuma kwa kasi masikioni na machoni mwa wengi kwa sasa nchini na nje ya nchi ya Tanzania.

Mara nyingi alipohojiwa amekuwa akisema kuwa muziki wa injiri nchini umekuwa ukihitaji ubunifu kila iitwapo leo maana katika dunia ya sasa hakuna tasnia ambayo imesinzia, kila moja iko macho na inaumiza kichwa kuja na vitu vipya.

"Watu ukiwaambia unaimba gospel music wanacheka na kubeza sana..wengine hawataki hata kusikia story yako inaishiaje, ni kwa sababu muziki huu umekuwa stagnant kama utamaduni flani usioenda na wakati uliopo. mimi nimeamua kuja na mrindimo tofauti na radha mchanganyiko ndani ya album moja hiyo hiyo #sinyamazi"  alisema.

''Redio nyingi zimekuwa kikwazo kikubwa cha kuinuka kwa muziki huu pia. tuna watu wenye vipaji katika uimbaji lakini wamekuwa wakitozwa pesa kubwa ili tu wimbo upigwe tena sio kila siku!!!''

Pia Danny Bandezu ameongeza kuwa miongoni mwa majipu makubwa nchi ni pamoja na mfumo mzima wa uzalishaji wa muziki nchini yaani kuanzia utunzi wa msanii hadi kurekodi na kisha promo na usambazwaji wa muziki wenyewe.

msanii kwa sasa anaimba na kurekodi kwa sababu tu kipaji kina muwasha huko ndani na kwamba hawezi kutulia mpaka amefanya kitu. sasa suala linakuja kwenye faida atakayoipata msanii huyu ni kwa namna gani katika mfumo huu? studio zinaku exploit, watangazaji wanakuchuna, msambazaji anakuja anakumalizia kabisa kwa kukwambia niuzie master cd yako kwa kiasi flani, kisha yeye anarudisha hiyo pesa mara mia kidogo na sio haki yako tena japo unavuma kila mtaa. hapa ndipo linapokuja suala la copyright society of Tanzania.
DANNY BANDEZU: Mwonekano wa nyuma ya cd cover lake kwa nyuma. hili ni cover la wimbo mmoja unaoitambulisha album yake mpya #sinyamazi
bonyeza link hii kujua maudhui mazima ya album hii na wimbo wa #sinyamazi wa #dannybandezu
https://www.youtube.com/watch?v=d6HZGhEev_Y

Comments

Popular posts from this blog

DANNY BANDEZU NI NANI?