DANNY BANDEZU NI NANI?

KUZALIWA
Amezaliwa mwaka 1985 08 august huko mjini mwanza, Tanzania. jina lake kamili ni Daniel joseph Itang'are. lakini amekuwa maarufu kwa jina la 'danny Bandezu'. wazazi wake ni Joseph itang'are ambaye ni mfanya biashara na mdau mkubwa wa soka nchini Tanzania, Mama yake ni Joyce seko Bogohe mtoto wa mwanasiasa maarufu Lameck makaranga Bogohe.

ELIMU
Danny Bandezu alianza elimu ya msingi mnamo mwaka 1994 - 2000 katika shule ya msingi Shamaliwa iliyopo eneo la igoma jijini mwanza, Tanzania.

Elimu ya sekondari aliipata katika shule ya mission imilikiwayo na kanisa maarufu la African inland church AIC iitwayo Bujora secondary school mnamo mwaka 2002 - 2005.

Baadae alijiendeleza katika elimu za juu kwa kuchukua kozi mbalimbali ikiwemo uandishi na utangazaji wa habari yaani journalism katika chuo cha habari cha Royal college kilichopo jijini Dar es salaam mwaka 2009.

Ameoa na ana watoto wawili Jemimah na Enrique Daniel.

MUZIKI
Danny alianza kujishughulisha na muziki tangu akiwa mdogo kwa kupenda uimbaji wa mwanamuziki marehemu jim reeves na ile christmas album yake. ilikuwa kila akitoka shule akiwa darasa la kwanza alikuwa akiiweka ile kanda ndipo anatafuta chakula huku akisikiliza na kuiga ile sauti ya jim reeves.

mwaka 2006 alipata mkataba wa kurekodi na studio ya reflex iliyopo mwanza. alirekodi album ya nyimbo 12 ambayo aliita Nitamsifu Bwana na wimbo uliompa kujulikana sana ni ulioitwa Mambo Bado ambao uko katiko mtindo wa ragga au dance hall. mara alipoanza kusali kanisa la Efatha ministry mwenge kilichomtambulisha zaidi ni huo wimbo mambo bado na ukabadili jina lake na kuwa 'mambo bado'. Hata hivyo hakufanikiwa kuingiza album hii sokoni kutokana na utaratibu mbovu wa tasnia na soko la muziki nchini.

mwaka 2015 alipata nafasi nyingine ya kufanya kazi na producer na mwanamuziki maarufu omary mkali mmiliki wa OM records, pia Boniface kachale mwanamuziki na mpiga saxophone/trumpet maarufu nchini na kimataifa.

walikubaliana kufanya album moja yenye nyimbo 6 ambayo inaenda kwa jina la #sinyamazi ambayo tayari imepata umaarufu hata kabla ya uzinduzi wake. wimbo sinyamazi unawahusu watu wanaojifanya wachungaji na kumbe sio yaani fake pastors. miongoni mwa nyimbo hizo ni sinyamazi, yuko Baba, heshima, mji mpya na zingine.

KAZI
Tofauti na muziki danny bandezu amewahi kuwa mwalimu wa computer yaani ict na ics kwa shule za english medium primary na secondary ikiwemo imani english medium school. pia amewahi kuwa mwalimu wa lugha ya kiingereza sehemu mbari mbari ikiwemo humpton learning centrre. Amewahi kufanya gazeti la utatu, trenet tv,Mchungaji,  startimes na pia azam media ltd.

MAWASILIANO
p.o. box 79467 dar es salaam, Tanzania.
cell; +255 713 035 611
bandezu@yahoo.com
facebook; danny bandezu
twitter@bandezu
instagram +danny bandezu
web; dannybandezu@blogspot.com




Comments

Popular posts from this blog